VIGEZO MUHIMU VYA KUJUMUISHWA 1

  • Watu walio na miaka kumi na sita na zaidi, ambao wamegunduliwa na kuthibitishwa kuwa wana ugonjwa wa selimundu (HbS/β+ thelassemia, au aina zingine za maradhi ya selimundu)
  • Angalau matukio 2 sio zaidi ya 10 ya maumivu makali ya selimundu katika miezi 12 kabla ya kutoa ridhaa ya ufahamu
    • Vinafafanuliwa kama vipindi vya maumivu makali, maradhi makali ya kifua, kusimama kwa sehemu za siri kwa muda mrefu bila ashiki ya ngono (priapism), au kuvimba kwa ini au wengu
  • Ikiwa unatumia hydroxyurea, dozi ya hydroxyurea lazima iwe thabiti kwa angalau siku 90 kabla ya kuanza matibabu ya kinasibu.

VIGEZO MUHIMU VYA KUONDOLEWA1

  • Kama una ujauzito au unanyonyesha
  • Kama umeratibiwa kuwekwa damu mara kwa mara kwa njia ya mishipa
  • Kama una matatizo ya ini,ugonjwa mbaya wa ini,ugonjwa wa kibovu cha mkojo au ugonjwa mbaya wa figo
  • Kama ulikumbana na tiba ya jeni hapo awali au kufanyiwa upandikizaji wa uboho au shina la seli hapo awali
  • Kama kwa sasa unapokea voxelotor, crizanlizumab, au L-glutamine
  • Kama kwa sasa unapokea matibabu ya viungo vinavyochochea ongezeko la damu (hematopoietic-stimulating agents)
  • Kutumia vidhibiti vikali vya CYP3A4/5 au vishawishi-mwili vikali vya CYP3A4