Maswali yanayoulizwa mara kwa mara & Rasilimali

Majibu kwa
Mashujaa

 / 
Je, ni nini kitafanyika nikiamua kuwa nataka kujiunga?

Kabla ya wewe kusajiliwa kikamilifu kama mshiriki katika RISE UP, timu ya matabibu watatathmini historia yako ya kimatibabu na afya yako ili kuhakikisha unaweza kushiriki. Angalia Kuamua Kusajili ili kupata mawazo mazuri ikiwa jaribio ni sawa kwako.

Je, matokeo ya awamu ya 2 yalikuwaje?

Awamu ya 2 ya utafiti wa RISE UP kote duniani ilionyesha uongezeka wa maana kitakwimu kwa viwango vya mwitikio wa himoglobini kwa muda wa wiki 12 na mitapivat ikilinganishwa na dawa mwigo.

Kwa jumla wagonjwa 79 walisajiliwa katika awamu ya 2 ya utafiti wa RISE UP duniani kote. Wakati wagonjwa 27 walipokea dawa mwigo, kulikuwa na wagonjwa 52 waliopokea mitapivat.

Mitapivat iliboresha viashiria vya kuharibiwa kwa seli nyekundu za damu na kuundwa kwa seli nyekundu za damu ikilinganishwa na dawa mwigo. Viashiria vya kuharibiwa kwa seli nyekundu za damu zinakuonyesha ni jinsi gani seli zako nyekundu za damu zina afya, na seli zingine za damu zinaundwa.

Mitapivat pia ilionyesha kupunguka kwa zaidi ya 50% ya matukio ya maumivu ya selimundu (SCPC) ikilinganishwa na dawa mwigo.

Je, unatumia watoa huduma wale wale waliotumika kwa awamu ya 2 na awamu ya 3?

Ndiyo, watoa huduma wale wale waliotumika katika awamu ya 2 watatumika katika awamu ya 3, na pia watoa huduma wengine zaidi.

Je, tumejua kwa kiwango gani kuhusu mitapivat?

Mitapivat imefanyiwa uchunguzi tangu Machi 2014.

Zaidi ya wagonjwa 700, ikijumuisha waliojitolea wenye afya, wametibiwa na mitapivat kwa magonjwa mbalimbali.

Mitapivat imefanyiwa utafiti kwa zaidi ya miaka 5.

Je, ni nini haswa “tiba inayobadilisha ugonjwa” inamaanisha kwangu? Je, hii inaweza kubadilisha asidi nasaba (DNA) yangu?

Mitapivat kama tiba inayobadilisha ugonjwa inaweza kuboresha ugonjwa wako, lakini haitabadili asidi nasaba (DNA) yako.

Je, nina uhakika wa kuwa kwa matibabu?

Wakati wa awamu ya 3 ya utafiti, kwa kila wagonjwa watatu wanaoshiriki, wawili watakuwa kwa mitapivat na mmoja atakuwa kwa dawa mwigo.

Hata hivyo, kuna kipindi cha utafiti kilichopanuliwa chenye dawa ya maelezo wazi ya hiari ya miaka 4 ambacho kila mtu anapokea mitapivat.

Je, mitapivat iko salama?

Lengo la utafiti huu wa awamu ya 3 ni kuona ikiwa mitapivat ni salama na yenye ufanisi.

Hakuna wagonjwa waliyokuwa kwa mitapivat au dawa mwigo waliokomeshwa matibabu kwa sababu ya madhara wakati wa utafiti wa awamu ya 2.

Katika tafiti yote ya mitapivat, madhara yaliyoonekana kwa 10% au zaidi ya wagonjwa yalijumuisha maumivu ya kichwa, kuhisi uchovu, kichefuchefu, maumivu ya viungo, na COVID-19.

Mitapivat inaweza kuathiri jinsi dawa zingine zinafanya kazi, na madawa mengine yanaweza kuathiri jinsi mitapivat inafanya kazi. Kumeza mitapivat na dawa zingine inaweza kusababisha madhara.

Zungumza na daktari wako kuhusu madawa ambazo unatumia kwa sasa (ikijumuisha madawa za kuagiza, madawa za kuuzwa dukani na virutubisho, na bidhaa yoyote iliyo na balungi). Daktari wako wa utafiti atakujulisha ni madawa gani yako salama ya kuendelea kutumia ukiwa kwa mitapivat.

Je, ninahitaji kushiriki katika utafiti kwa muda gani?

Ukisajiliwa, kushiriki katika utafiti wa awamu ya 3 ni mwaka moja.

Je, mnasajili wagonjwa wapya katika awamu ya 3?

Ndiyo, na tungependa ujiunge na harakati. Jisajili hapa.

Je, hi hospitali gani zinashiriki katika awamu ya 3?

Kenya

  • KEMRI USAMRUNambari ya mawasiliano: 254721996988
  • Kondele Children's HospitalNambari ya mawasiliano: 254714481488
  • Strathmore UniversityNambari ya mawasiliano: 254733813613
  • KEMRI/CRDR Siaya Clinical Research AnnexNambari ya mawasiliano: 254722205901
  • Victoria Biomedical Research Institute (VIBRI)Nambari ya mawasiliano: 254720597654
  • KEMRI CRDR Clinical Research Clinic NairobiNambari ya mawasiliano: 254724522474
  • Gertrude's Children's HospitalNambari ya mawasiliano: 254721245721
Je, “inayodhibitiwa na dawa mwigo, kupofushwa mara mbili” ina maana gani?

Dawa mwigo ni kidonge kinachofanana kabisa na dawa ya utafiti lakini haina dawa yoyote amilifu. Dawa mwigo zinapeana njia ya kulinganisha matokeo yanayosababishwa na dawa ya uchunguzi. “Kupofushwa mara mbili” ina maana kuwa si wewe wala daktari wako mtajua ikiwa unatumia dawa mwigo au dawa ya utafiti, ili isiathiri matokeo au tathmini.

Je, faragha yangu italindwaje?

Kwa muda waote wa utafiti, jina lako na taarifa yote ya kimatibabu ya kibinfasi zitawekwa siri kamwe. Kila mshiriki katika utafiti watapewa kitambulishi maalum. Rekodi na data zilizokusanywa wakati wote wa utafiti hazitakuwa na jina lako au taarifa ya kukutambulisha binafsi, lakini kitambulishi cha kibinafsi.

Je, ni nini ninaweza kutarajia wakati wa utafiti?

Una mambo mengine yanayofanyika maishani mwako, na kupambana na ugonjwa wa selimundu kila siku ni changamoto kubwa. Ikiwa unahitaji usaidizi wakati wa utafiti, usaidizi unaweza kupatikana kwa:

  • Watunzaji
  • Utunzaji wa watoto
  • Usafiri
  • Usafirishaji
  • Ujira
  • Wauguzi kwa ziara za mbali
  • Ziara za mitandaoni

Huduma zilizopo hapo juu zinalingana na miongozi ya eneo na kitaifa. Tafadhali angalia na mtafiti wako wa eneo kudhibitisha ni huduma gani zinapatikana katika eneo lako. Taarifa zaidi kuhusu usaidizi utapatikana katika tovuti yako maalum ya usajili.

Moja ya motisha (ya kupigana) yangu kubwa ni watu katika jamii ya selimundu.

Teonna,

Shujaa wa Selimundu

@sicklequeent