Hadithi za Mashujaa

Kila Shujaa Ako na Hadithi

Teonna, Sickle Cell Warrior
TEONNA

Ninabaki mwenye tumaini kwa siku zijazo kwa kuendelea kujihusisha katika jamii ya Mashujaa.

https://www.instagram.com/sicklequeent/ @sicklequeent

S: Je, ina maana gani kwako kuwa Shujaa wa Selimundu?

J: Kwangu, Kuwa Shujaa wa Selimundu inamaanisha kuwa na nafasi ya kushinda changamoto nyingi tunazokumbana nazo na ugonjwa huu.

S: Kwa nini uINUKE (RISE UP)?

J: Kila wakati mimi hutafuta njia za kusaidia vitu viwe bora kwa Mashujaa wanaokuja baada yangu. Tiba mpya na jaribio za kimatibabu zilizo na uwezo wa kufanya mambo yawe bora zinanifanya niwe na furaha zaidi.

Tristian, Sickle Cell Warrior
TRISTIAN

Kama Mashujaa, tunajipigania na kwa kila mmoja.

S: Je, ina maana gani kwako kuwa Shujaa wa Selimundu?

J: Ninajivunia kuwa ninapeana sauti kwa kizazi kichanga wenye selimundu. Nimewaonyesha watu wengi kuwa wamekosea ikija kwa kile ambacho ninaweza kufanya.

S: Kwa nini uINUKE (RISE UP)?

J: Mashujaa wanakuwa na nguvu zaidi wakiwa pamoja. Tukilenga maendeleo yanayofanywa, hatutaruhusu selimundu kufanya tuwe watu aina fulani.

Dominique, Sickle Cell Warrior
DOMINIQUE

Kama Shujaa, nabakia mwenye tumaini na nakataa kuishi nikiwa na uoga.

https://www.twitter.com/sickle1000/ @sickle1000

S: Je, ina maana gani kwako kuwa Shujaa wa Selimundu?

J: Kuwa Shujaa ni kuhusu uvumilivu. Mimi hujaribu kutumia kila siku vizuri, licha ya jinsi selimundu yangu hunifanya nihisi. Na hiyo imenifanya niwe mwenye nguvu zaidi.

S: Kwa nini uINUKE (RISE UP)?

J: Ni muhimu kujiunga na jaribio za kimatibabu kama RISE UP kwa sababu ni kuhusu kuweka watu wenye selimundu kwanza na kuelewa mtazamo wetu. Kadiri ya jamiii ya Mashujaa wanavyojishughulisha zaidi, fursa nyingi zinapatikana.

Golie, Sickle Cell Warrior
GOLIE

Kuwa Shujaa wa Selimundu inamaanisha kuwa wewe ni mpiganiaji.

https://www.instagram.com/golielorenzo/ @golielorenzo

S: Je, ina maana gani kwako kuwa Shujaa wa Selimundu?

J: Naangalia Mashujaa wenzangu na ninachangamshwa. Sisi sote tunalenga kupigania nafasi za kusaidia kutusukuma mbele. Kama kuna nafasi yoyote na maisha na selimundu kuwa tofauti kesho kuliko jinsi nimekumbana nayo leo, basi siku zote itanipa matumaini.

S: Kwa nini uINUKE (RISE UP)?

J: Ni muhimu kuwa tunashiriki katika jaribio za kimatibabu kama RISE UP, si kwa sababu yetu kibinafsi, lakini kwa jamiii kubwa ya Mashujaa. Tunapata kuhakikisha kuwa kizazi kijacho cha Mashujaa ya Selimundu kinakuwa na fursa bora za kiafya.

Mia, Sickle Cell Warrior
MIA

Mashujaa wanakabiliana na ugonjwa wa selimundu kwa uwezeshwaji.

S: Je, ina maana gani kwako kuwa Shujaa wa Selimundu?

J: Kuwa Shujaa ni kuhusu kufanya kazi ili kushinda changamoto. Unajaribu kutoacha selimundu ikukomeshe, hata katika siku zile ngumu zaidi.

S: Kwa nini uINUKE (RISE UP)?

J: Ninataka kusaidia Mashujaa kupata fursa za kupata afueni. Jaribio za kimatibabu kama RISE UP zina uwezo wa kubadilisha jinsi tunakumbana na selimundu. Yote ni juu ya kuturuhusu kufanya kazi na kutunza familia zetu, kuwa na wakati mwafaka na wapendwa wetu, na kufurahia maisha yetu kwa jumla.

Blaze, Sickle Cell Warrior
BLAZE

Piga kelele. Kwenda kwa nguvu. Kuwa na sauti kubwa. Tetea. Hatutaachwa nyuma.

https://www.instagram.com/highplaceblaze/ @highplaceblaze
DeMetrious, Sickle Cell Warrior
DeMITRIOUS

Kujiunga na RISE UP kama Shujaa wa Selimundu kumenionyesha nguvu ambazo sikujua niko nazo.

S: Je, ina maana gani kwako kuwa Shujaa wa Selimundu?

J: Kama Shujaa wa Selimundu, sisi ni wa kipekee kweli. Tuna nguvu kwa sababu lazima tuwe. Inanipa matumaini ya siku zijazo nikijua kuwa nafanya sehemu yangu katika kujisaidia, na wengine wanaoishi na selimundu.

S: Kwa nini uINUKE (RISE UP)?

J: Ni muhimu kuwa jasiri, kuzungumza kwa niaba ya ugonjwa wa selimundu, na kuwa kimbele.