Kuamua Kujisajili katika Jaribio la Kimatibabu ya Selimundu

Kile Ambacho Kinahitajika Kujiunga na Rise Up

Teonna, Sickle Cell Warrior
TEONNA,

Shujaa wa Selimundu

Sababu Rise Up Inaweza Kuwa Inakufaa

Vigezo vya Kustahiki:

  • Uko na umri wa miaka 16 au zaidi
  • Umetambulika kuwa na selimundu
  • Ikiwa wewe au mwenzi wako mna uwezo wa kuwa mjamzito, lazima ukubali kutumia aina 2 za vidhibiti ujauzito
  • Umekuwa na angalau matukio 2 lakini isiyozidi 10 ya maumivu katika mwaka uliopita
    • Imefafanuliwa kama maumivu yanayohitaji kuangaliwa na mtabibu na matibabu yanayosababishwa na ugonjwa kali wa kifua, kusimama kwa mboo unaoendelea, au vizuizi vya seli nyekundu za damu kwenye ini, bandama, au mahali pengine mwilini
  • Una viwango vya himoglobini kati ya gramu/desilita 5.5 na 10.5
  • Ikiwa unatumia hydroxyurea kipimo lazima kibaki sawa kwa angalau siku 90 kabla ya kuanza dawa hii ya utafiti
DeMitrious, Sickle Cell Warrior
DeMITRIOUS,

Shujaa wa Selimundu

Sababu Rise Up Haiwezi kuwa Inakufaa

  • Ukiwa mjamzito au unanyonyesha
  • Ukiwa unapokea damu mara kwa mara kwa njia ya mishipa iliyoratibiwa
  • Ukiwa na matatizo ya ini na nyongo, ikijumuisha magonjwa ya ini au kibofu cha nyongo
  • Ukiwa na ugonjwa kali ya figo
  • Ukiwa umepata tiba ya jeni au umekuwa na upandikizaji wa uboho au seli za shina
  • Ukiwa kwa sasa unapokea matibabu ya ugonjwa wa selimundu (kama vile voxelotor, crizanlizumab, au L-glutamine), isipokuwa na hydroxyurea
  • Ukiwa kwa asasa unapokea tiba za kusisimua kutengenezwa kwa damu, kama vile erythropoietin

Kuwa na ushiriki wa juu katika jaribio za kimatibabu unasaidia kupeana uwazi kuhusu machaguzi na fursa zinazopatikana kwetu. Ni ya manufaa kwa uzuri wa wengi.

Golie,

Shujaa wa Selimundu

@golielorenzo